LOWASA KUGOMBEA URAISI 2015"MAONI YA WANAFUNZI UDOM"
Waziri Mkuu aliyejiuzuru na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Ngoyai Lowasa alipotembelewa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha DODOMA (UDOM) ambao walitokea katika shule zasekondari za kata.
Wanafunzi hao, pamoja na kumpongeza Mh. Edward Lowassa kwa kuasisi na kusimamia ujenzi wa shule za sekondari katika ngazi ya kata pia wamemtaka achukue fomu za kugombea urais 2015 muda utakapowadia. Pia wameahidi kujichangisha
fedha kwa ajili ya malipo ya fomu hizo endapo italazimika