M 2 THE P AMETOKA HOSPITAL

Msanii M2 THE P ambaye alikuwa na Ngwea siku umauti unamkuta ametoka hospital.Msanii huyo ambaye alifikishwa hospitali akiwa hajitambui na hali yake kuwa mbaya sana mpaka kufikia kupelekwa wodi ya wagonjwa mahututi katika moja huko Afrika kusini ambako walikuwa kwa shughuli za mziki.
Taarifa  zinasema kuwa kwa sasa anaendelea vizuri sana hali inayotia matumaini kinachotakiwa ni dua za watanzania wenye mapenzi mema kwake.
M 2 THE P mpaka sasa hajui taarifa za Kufa kwa rafiki yake kipenzi Albert Mangwea kilichotokea wakati wapo pamoja chumbani.
Mwanadada huyo ilibidi amtanie M 2 THE P kwa kumwambia "ukirudi bongo mwambie Ngwea nina kesi nae kwanini kaondoka bila kuniaga" hali iliyopelekea kumfanya M 2 THE P asijue lolote linaloendelea mpaka sasa.


PICHANI NI MWANADADA MAGIE NA M 2 THE P WAKITANIANA BAADA YA KUMTEMBELEA NYUMBANI.



Share: