MAOMBI ZAIDI KWA MANDELA NJE YA HOSPITALI ALIPOLAZWA

Mamia ya watu wanaendelea kukusanyika nje ya hospitali alikolazwa Nelson Mandela mjini Pretoria Afrika Kusini. Inaarifiwa Mandela bado yuko hali mahututi.
Wamekuwa wakimuimbia nyimbo na kumuombea nje ya hospitali. Wengine wamekusanyika katika iliyokuwa makaazi ya Mandela mtaani Soweto.

Afrika Kusini
Watu wana wasiwasi kuhusu hali y mandela lakini pia wanataka kuonyesha wanavyojivunia kiongozi wao ambaye wanamuona kama baba wa taifa lao.
Mandela , rais wa kwanza mweusi Afrika Kusini, anaugua maradhi ya Mapafu.
Mamia ya wananchi walikesha kwa maombi maombi nje ya makaazi ya zamani ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Nelson mtaani Soweto.
Rais Jacob Zuma amesema kuwa afya ya shujaa huyo aliyepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo inaendelea kuimarika.
Mandela aliye na umri wa miaka 94 amekuwa hospitalini akiuguwa ugonjwa wa maambukizi ya mapafu.
Awali mwanawe wa kike, Makaziwe alisema afya ya babake inaendelea kuwa njema.
Aidha Makaziwe amevikashifu vyombo vya habari kwa kukita kambi nje ya hospitali alikolazwa shujaa huyo akisema wanahabari wanapaswa kumheshimu babaake.
Rais Jacob Zuma alisema Alhamisi kuwa hali ya Mandela iliimarika lakini bado yuko hali mahututi.
"leo angalau yuko sawa kidogo kuliko nilivyomwacha jana usiku,'' alisema Rais Zuma baada ya kuongea na madakatari wanaomtibu Mandela.
Bwana Zuma alifutilia mbali safari yake ya Msumbiji ili kumtembelea Mandela hospitalini.
Wakati huohuo mwanawe Mandela Makaziwe alisema Mzee 'bado yupo' na kuwa anaweza kuhisi mtu akimgusa.



Share: