Rais wa Marekani Barack Obama leo Ijumaa anaelekea Afrika Kusini ambapo miongoni mwa shughuli zake atazuru kisiwa cha Robben Island alikofungwa jela rais wa zamani Nelson Mandela kwa miaka 27.
Rais Obama anakwenda nchini humo wakati bw. Mandela akiwa katika hali mbaya ya afya. Rais huyo wa zamani anatibiwa katika hospitali moja ya Pretoria.
Alihamis rais Obama alisema ziara yake katika eneo ambalo watumwa wa Afrika waliondoka barani humo kwenda Amerika kaskazini imempa hamasa mpya ya kulinda haki za binadamu. Bw. Obama alitembelea kisiwa cha Goree kwenye ufukwe wa Senegal Alhamis.
Wanahistoria wanasema maelfu ya Waafrika wanaume kwa wanawake wakiwa wamefungwa minyororo walishikiliwa huko na kupitia kile kilichoitwa mlango wa kutorudi tena kupanda meli ya watumwa wakielekea bahari ya Atlantic.
Rais Obama alisema ziara yake katika kisiwa hicho ilimpa hisia kali na nafasi ya kutathmini upya biashara ya utumwa katika karne ya 16 na 19