Picha 25- SAFARI YA MWISHO YA ALBERT MANGWEA MJINI MOROGORO

Hakika Albert Mangwea alikuwa ni mtu wa watu maana si tu kwa dar hata morogoro watu wengi walifika kuusindikiza mwili wa msanii huyo.
Kati ya tukio lililowahudhunisha wengi ni baada ya msanii mwenzake na aliyekuwa rafiki wa karibu wa Ngwea M 2 THE P kufika kuuaga mwili wa rafiki yake.Aliangua kilio kilicholeta simanzi kubwa kwa watu waliokuwepo eneo la tukio.Naweza sema katika misiba yote ya wasanii huyu ni msanii pekee aliyebeba watu wengi sana.
Hakuna ripoti ya mtu kupoteza maisha katika zoezi zima la kuuaga mwili wa msanii huyo.Katika hotuba zilizosomwa na baadhi ya wawakilishi wa vyombo mbalimbali walielezea jinsi Ngwea atakumbukwa kwa mchango wake katika muziki na sanaa ya Tanzania kwa ujumla.
Kitu kizuri zaidi kilichojionyesha kwenye msiba wa msanii huyu ni ushirikianao alioupata toka kwa wasanii wenzake wa tasnia mbalimbali hapa nchini.

MUNGU AMUWEKE PEMA PEPONI ......amen





















H
Share: