"TUZO MOJA NAMPA HAYATI ALBERT MANGWEA"-KALA JEREMIAH

Kala Jeremiah ndio msanii aliyechukua tuzo tatu katika tuzo za kill music award zilizofanyika mapema mwisho wa wiki iliyopita.Akiwa ameshikilia tuzo tatu mkononi,ametoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa tuzo yake moja anaipeleka kwa Albert Mangwea ikiwa ni heshima kwakuwa Marehemu alikuwa anafanya muziki kama anaofanya yeye.
Taarifa hiyo ameitoa kupitia ukurasa wake wa face book
Kala amesema hivi soma hapa chini......

"tAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA KWA UJUMLA.
mIMI KAMA MSANII BORA WA HIP HOP KWA MWAKA HUU NAPENDA KUCHUKUA MUDA HUU KUWATANGAZIA WATU WOOTE KUWA. KATIKA TUZO TATU NILIZOCHUKUA MOJA NAIKABIDHI KWA ALBERT MANGWEA.YANI NI TUZO YA MANGWEA NA NITAIPELEKA KWA MAMA MZAZI WA MANGWEA MOROGORO.
NIMEAMUA HAYO KWA KUWA HAYATI ALBERT MANGWEA ALIKUWA ANAFANYA MZIKI AMBAO UKO UPANDE AMBAO MIMI NIMESHINDA TUZO TATU YANI HIP HOP.
TUZO NILIYOAMUA KUMPA MANGWEA NI TUZO YA MSANII BORA WA HIP HOP. KWA KUWA ALIKUWA ANASTAHILI PIA KUITWA HIVYO.
TUZO HII NAAMINI ITAKUWA UKUMBUSHO MHIMU SANA KWA FAMILIA YAKE.LAKINI PIA ITAKUWA INAONYESHA MSHIKAMANO WETU KAMA WASANII WA HIP HOP.
POPOTE ULIPO KAMA WEWE NI SHABIKI WA HIP HOP TAFUTA NJIA YOYOTE YA KUENDELEA KUMUENZI NDUGU YETU
MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI HIP HOP.
KALA JEREMIAH AKIWA ANAPOKEA TUZO SIKU YA KILL MUSIC AWARDS
MAREHEMU ALBERT MANGWEA ENZI ZA UHAI WAKE AKIWA ANAPAFOM
Share: