Skip to main content

(Angalia Taarifa ya kusikitisha)BINTI AKATWA KATWA NA MAPANGA


Mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Kizega wilayani Iramba Bi. Mariamu Alphonce mwenye umri wa miaka kumi ameuwawa kikatili kwa kukatwa shingo na kucharangwa kwa panga sehemu mbalimbali za mwili wake na kaka yake bwana Elibariki  Alphonce.


Akieleza kwa uchungu baba wa mtoto huyo bwana Alphonce Msengi amesema alipofika nyumbani kwake majira ya saa kumi na moja jioni alikuta damu nyingi na alipo angali vizuri alimuona mtoto wake Mariamu Alphonce akiwa amekatwakatwa kwa mapanga na tayari alikuwa ameshafariki.

Bwana Msengi baada ya kuona hivyo alipiga yowe na walikuja majirani na watoto na wakamwambia tumemuona mtoto wako Elibariki akiwa na mapanga mawili akikimbia huku akiwa hana nguo. Wakieleza mwenyekiti wa kitongoji Bi Vailet Mbigu na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kizega bwana Elisante Gyuzi wamesema pamoja na shule kuandaa taratibu zote za mashishi , kijana aliyefanya unyana huo huwa anavuta bangi na mara nyingi alikuwa akisikika kumtishia kumuuwa baba yake kwa kumkata kwa panga.

Kwa upande wake  kaimu mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Iramba daktari Timoth Sumbe amesema wamempokea Mariamu Alphonce akiwa ameshafariki huku mwili wake ukiwa na majeraha ya kukatwakatwa sehemu ya shingoni,kichwani.

Akiongea kwa simu kamanda wa jeshi lapolisi mkoani Singida bwana Godfrey Kamwela amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na jeshi lake lina endelea kumsaka mtuhumiwa bwana Elibariki Alphonce ambaye alitoweka baada ya mauaji ili aweze kufikishwa mahakamani.

Popular posts from this blog

(DjMix) DJ DEO - BONGO FLEVA HITS NON STOP MIXING

Please listen and download this dj mixing from tanzania by group YOUNG DJS ...Present Dj Deo on this mix

(Audio - Dj Mixing) DjDeo - BONGO FLEVA OLD SKOOL NON STOP

This is mix from the Dj in Tanzania who representing YOUNG DJS GROUP ... Make this olds of bongo fleva ....
Take your time to download and to listen of it...If you will like the mix yu can subcribe and comment below or to my whatsapp number.... on the cover ...

KURASA ZA MAGAZETI MBALIMBALI ZATAWALA PICHA ZA MANDELA

Baada ya hapo jana majira ya saa 2 usiku kwa saa za afrika ya mashariki kutangazwa kifo cha aliyekuwa mpigania uhuru na raisi wa kwanza wa Afrika kusini Bw.Nelson Mandela,leo hii magazeti mbalimbali duniani yatawala kwa habari hiyo

ANGALIA MAGAZETI HAYO