Exclusive-MISTARI YA KARIBU DAR-KALA JEREMIAH

sONG: KARIBU DAR

intro: BROTHER TUMA EEE NGOJA KWANZA EE
PRODUCER MBEZI YOOH HAHA 0444 SMART MUSSIC

ubeti wa kwanza

pICHA LINAANZA KA MOVIE YA SOLOMON
GHAFLA VUMBI LINAZIDI WAJANJA WANAVAA MIWANI
HII NDO DAR KARIBU ILA USIJISIKIE NYUMBANI
HAPO UBUNGO USINUNUE SIMU UTAUZIWA SABUNI
PANDA DALADALA TUKUTANE BUGURUNI
KUNA WATU WANAPIGA NDOLE UTADHANIA MAJINI
KA NI USIKU UTAONA RANGI ZOOTE ZA BIKINI
WANAUZA MWILI ILI WANUNUE WALI MAINI
USICHEKE BRO KWA SABABU MI SIYO MR BEAN
CHUNGA WALLET HAPA KUNA WIZI WA MFUKONI
HAUKAWII KUSHUKA KWENYE GARI HAUNA PHONE
KUWA MAKINI UVUKAPO HUKU GARI HAZIPIGI HONI
DALADALA ZINA......... BAJAJI INAKESHA MACHO
KA HUAMINI NGOJA USIKU ILI UAMINI WE TOMASO
WASIO NA KAZI WANASHINDIA STORY ZA FREEMASON
WAJANJA WAMEPANGA SINZA KINO NA TABATA
MCHANA ANAZIBUA VYOO USIKU ANAKULA BATA
USIKOJOE OVYO BRO MGAMBO WATAKUKAMATA
HII NDO DAR MBONA UNADATA KABLA HATA HUJAPATA STATER?

kiitikio:

BATA NI DAILY, DAILY, KARIBU BUSH MEN KAA CHINI TUKUPASHE HABARI, SHANGAA MATAA DAR UGONGWE NA GARI (DAR ES SALAM YA SASA)
DAILY DAILY KARIBU BUSH MEN KAA CHINI TUKUPASHE HABARI
SHANGAA MATAA DAR UGONGWE NA GARI
(DAR ES SALAM YA SASA)

ubet wa pili

KARIBU SANA KWENYE HILI JIJI LA JOTO
USWAHILINI CHUMBA KIMOJA BABA MAMA NA WATOTO
SI ULISIKIAGA MABOM YA GONGO LA MBOTO?
YALIFANYA RAFIKI YANGU WA DAMU AKAFIA GETO
YALIACHA KOVU KUBWA KAMA LA MBAGALA
DAR ES SALAM WATU WENGI TU HAWANAGA PA KULALA
KAMA UNATAKA MILUNGI TWENZETU MITAA YA ILALA
MAGOMENI NA UJANJA WANGU WOOTE NILIITWA FALA
WATU WANAINGIZA PESA WAKIWA GETO WAMELALAAA
WATU WENGI TOKA WAJE HAWAJAWAHI KURUDI KWAO
SABABU HAWANA NAULI JAPO WAMEMISS NDUGU ZAO
KUHUSU KUSHINDA NA NJAA HAPA NDO ZAO
WAUZA SURA WANAISHI KWA KUWAUZA MADEM ZAO
MAMA ANAUZA BANGI, BABA AMEKATA RINGI, ANASHINDA ANACHEZA BAO
WAKE ZAO WANAZINI KULISHA WATOTO WAO
VIJANA WAO WANATEMBEZA KARANGA, WANATEMBEZA MAJI,WANATEMBEZA VOCHA SIYO KWA MITAJI YAO
JIONI WANAKABIDHI HESABU KWA BOSS WAO
HII NDO DAR UKIPENDA UNAWEZA KUIITA BONGO
MACHIZI WAKIKOSA HELA YA BIA WANAKULA GONGO
SIRI HAIWI SIRI USWAHILINI UKIPATA MCHONGO
WAPANGAJI WATAKUANDAMA BRO MPAKA UTAHAMA JENGO
NI MAJUNGU MIXA WANGA UTAENDA TU KWA MGANGA UTAPOLALA GETO KWAKO KISHA UKAMWAGIWA MCHANGA

rudia kiitikio

ubeti wa 3

DAR ES SALAM INGEKUWA NCHI RAIS ANGEKUWA LOWASA
HUKU WATU WASHASHITUKIA KUNA MCHEZO KWENYE SIASA
USIONE WATU WAMEPENDEZA WENGINE HAWANA HATA MIA
HAPA MBOGA NI MAHARAGE NYANYA CHUNGU NA BAMIA
BROTHERMEN ANATEMBEA TOKA KEKO KWA MIGUU
ANAKWENDA MLIMAN CITY KUNUNUA MKATE TU
(R U ON FACEBOOK?) NDO MASWALI YA MADUU
UKITAKA DEM WA PEKE YAKO KATA MGOMBA LALA JUU
UKIMWITA DEM WAKO BAR WANAKUJA CREW
UTACHUNWA MPAKA RABA UBAKI MIGUU JUU
HAPA BOMBA HALIJATOWA MAJI MWEZI MZIMA
HII NI USWAHILINI TU WALA SIYO KWA JIJI ZIMA
TWENDE MBEZI AU MASAKI YANATOKA MWAKA MZIMA
KATIZA KWA MTOGOLE UPORWE SIMU MCHANA
SIKU HIZI MWANAUME ANAVAA SURUALI YA KUMBANAAAAAA!
SIKU HIZI DADA YAKO ANA KALIO ZA KICHINA
UKIMTAFUTA HUMPATI ASHABADILI RANGI NA JINA

rudia kiitikio


Popular posts from this blog