UWANJA WA TAIFA WAKABITHIWA RASMI KWA SERIKALI

Serikali imesema kuanzia sasa itafuatilia kwa karibu ukusanyaji wa mapato yanayotokana na viingilio vya mechi za soka zinazochezwa kwenye Uwanja wa Taifa.

Jana serikali ya China iliukabidhi rasmi Uwanja wa Taifa kwa serikali baada ya ujenzi wake uliodumu kwa miaka 7 na kugharimu zaidi ya Sh 60 Bilioni za Tanzania kukamilika.

Uamuzi huo wa serikali, unafuatia kuwapo kwa maswali ya mara kwa mara kutoka kwa wadau wa michezo ambao wamekuwa wakihoji uchache wa fedha zinazotangazwa baada ya mechi zinazopigwa kwenye uwanja huo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa uwanja huo Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni naMichezo,Fenella Mukangara alisema,hatua hiyo itasaidia kudhibiti upotezi wa mapato unaosababishwa na watu wasio waaminifu.

“Nasema serikali itafuatilia kwa karibu kuanzia suala la kudhibiti idadi ya watu wanaoingia uwanjani na mapato yanayotokana na viingilio,”alisema Mungangara na kuongeza;

“Kama uwanja unachukua watu 15 badi idadi hiyo hiyo ndiyo waingie na mapato yatakayopatikana yafanane na uwingi wa watu,”.

Pia,aliishukuru serikali ya China kwa kukukabili maombi ya serikali ya Tanzania na kujenga uwanja huo wenye hadhi ya kimataifa.

“Tunaishukuru sana serikali ya China kwa mchango wake wa fedha na sisi sasa tupo kwenye ramani ya dunia kutokana na kuwa na uwanja huu ambao hata tevevisheni za kimataifa kama Super sport imekuja hapa na kututangaza duniani kote,”.alisema Mukangara.

Naye,Balozi wa China hapa nchini,Luo Youging akizungumza wakati wa makabidhiano hayo,alisema ni matumaini yake serikali ya Tanzania na watu wake itautumia uwanja huo kuendeleza michezo nchini.

“Sasa vijana Watanzania watajenga afya zao kwani uwanja huu unakidhi mahitaji yote muhimu ikiwemo soka na riadha,pia Tanzania itajulikana duniani kote kutokana na kuwa na uwanja wenye hadhi ya kimataifa,”.alisema Youging.


Share: