Makala ndogo-TBC YACHAPIA-"OBAMA RAISI WA TANZANIA"

I ngawa inajulikana kuna makosa mengi kwa binadamu.Sio tatizo sana kwa binadamu kukosea kutamka neno fulani na kutamka vingine.Ieleweke kwamba mwandishi wa habari pia ni mwanadamu hivyo kukosea kwake ni jambo la kawaida.
Lakini kwa mtazamo wa watu wengi ni kuwa kuna baadhi ya watu au chombo fulani kikikosea jambo inakuwa ni hadithi kubwa sana wakidhani kuwa hawawezi kukosea.Dhana hiyo si kweli.

Hivyo ndio kama chombo kikubwa cha habari nchini na shirika la utangazaji Tanzania(TBC) walipokosea kuandika cheo cha raisi wa Marekani aliyetembelea nchini jana kuamkia leo.TBC ilikosea kuandika kuwa OBAMA - RAISI WA MAREKANI nayo ikaandika OBAMA RAISI WA TANZANIA.

Hapo ieleweke kwamba mtu anapokosea ni kuwa maneno mawili yanakuwa yanaingiliana .Pengine mwandishi alitaka kuandika sahihi lakini kutokana na kuingiliana na maneno ikabidi achapie hivo.

CHEKI TBC ILIVYOANDIKA


Share: