MPIGANAJI WA UHURU AFUTWA KAZI AFRIKA KUSINI

Rais Jacob Zuma, wa Afrika Kusini, amemfuta kazi waziri wake wa nyumba na mkereketwa na vita dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo Tokyo Sexwale.
Bwana Sexwale ni mmoja wa mawaziri ambao watapoteza nyadhifa zao katika kile rais Zuma, alichokitaja kama mpango wa kuimarisha huduma za serikali.
Wachanganusi wa masuala ya kisiasa hata hivyo wanasema kuwa Bwana Sexwale amefutwa kwa kuwa alihusika na kampeini ya kumuondoa rais Zuma mwaka uliopita.
Sexwale alifungwa katika gereza la Robben Island pamoja na rais wa kwanza wa nchi hiyo Nelson Mandela.
Yeye ni pia afisa wa ngazi ya juu wa shirikisho la mchezo wa soka duniani Fifa

PICHANI NI TOKYO SEXWALE


Popular posts from this blog