WATUHUMIWA WA BOKO HARAMU WAFUNGWA KIFUNGO CHA MAISHA

Wanachama wanne wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Kiislamu la Boko Haram, wamehukumiwa kifungo cha maisha gerezani, baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika na mashambulio ya bomu yaliyosababisha vifo vya watu kumi na tisa.
Wanne hao walipatikana na hatia ya kupanga na kutekeleza mashambulio ya mabomu katika ofisi za tume ya uchaguzi na kanisa moja mwaka uliopita.
Hukumu hiyo ndiyo kali zaidi kuwahi kutolelwa kwa mwanachama au mshukiwa yeyote wa kundi hilo la Boko Haram.
Kundi hilo limehusika na mashambulio kadhaa ambayo yamesababisha maafa mengi katika maeneo ya Kaskkazini na Kati nchini Nigeria.
Katika miaka ya hivi karibuni kundi hilo limekuwa likiwalenga raia wa kawaida na zaidi ya watu elfu mbili wameuawa tangu kundi hilo la Boko Haram kuanzisha uasi mwaka wa 2009, katika juhudi zake za kutaka kuundwa kwa taifa jipya la Kiislamu katika eneo lililo na idadi kubwa ya Waislamu Kaskazini mwa Nigeria.
Hali ya hatari, ilitangazwa tarehe kumi na nne mwezi Mei mwaka huu, katika majimbo ya Kaskazini Mashariki ya Adamawa, Borno na Yobe, hatua iliyoishurutisha serikali ya nchi hiyo kutuma zaidi ya wanajeshi elfu mbili kushika doria katika eneo hilo na pia kuvunja kambi za wanamgambo hao.
Utawala wa nchi hiyo umesema, kuwa washukiwa kadhaa wa kundi hilo wamekamatwa na wachache tu wamefikishwa mahakamani.

Washukiwa hao wanne walipatikana na hatia ya kupanga shambulio la bomu katika ofisi za tume ya uchaguzi katika eneo la Suleja katika jimbo la Niger, na kusababisha vifo vya watu kumi na sita na shambulio lingine Julai mwaka huo dhidi ya kanisa moja nchini Bofya Nigeria.
Mshukiwa mwingine wa tano alihukumiwa kifungo cha miaka kumi gerezani huku mshukiwa mmoja akiachiliwa huru na mahakama.
Siku ya Jumatatu Uingereza, ilijumuisha kundi hilo la Bofya Boko Haram miongoni mwa makundi yanayokisiwa kuwa ya kigaidi na mtu atakayetoa usaidizi kwake atakuwa amevunja sheria na kukisiwa kuunga mkono ugaidi.
Kundi hilo ambalo, jina lake lina maana, ''Elimu ya nchi za Magharibi hairuhusiwi'' limesema nia yake kuu ni kupindua serikali ya Nigeria na kuunda taifa la Kiislamu.
Kundi hilo limelenga mashule na tayari limeteketeza kadhaa tangu mwaka wa 2010.
Siku ya Jumapili wanafunzi ishirini na wawili wa shule moja katika jimbo la Yobe waliuawa na watu wanaoaminika kuwa wapiganaji wa kundi hilo.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema baadhi ya wanafunzi hao, walichomwa wakiwa hai huku wengine walipigwa risasi walipokuwa wakitoroka


Share: