MZEE MAGARI AINGIA RASMI KATIKA MUZIKI

CHANZO CHA HABARI NA MILLADAYOWiki kadhaa zilizopita msanii wa bongomovie Rose Ndauka alishirikishwa kwenye collabo na kundi la TNG Squard kwenye wimbo wao mpya, baada ya hapo idadi ya wasanii wa bongomovie ambao wanafanya muziki ilizidi kuongezeka wakiwafuata wakina Snura na Shilole.
Leo hii msanii mkongwe na maarufu sana kwa kuigiza kama mtu katili au wakati mwingine mtu tajiri Mzee Magari, ametoa wimbo wake unaitwa “Dar Raha” ambapo kwenye interview na millardayo.com Mzee Magari anasema “Ninampango wa kuifanya fani hii ya muziki kuwa serious kama ilivyo kwa upande wa movie, sijatoa huu wimbo kwa kujifurahisha bali muziki pia ni kitu ninachokipenda…. kuna baadhi ya wasanii wanafahamu historia yangu na muziki kabla hata sijaanza kuigiza movie“.
Sasa basi mtu wangu wa nguvu hii ni nafasi yako kusikiliza hiyo ngoma ya Mzee Magari kwa mara ya kwanza exclusive hapa kwenye millardayo.com na utoe maoni yako pia manake mwenyewe atapita baadae kuona watu wamepokeaje..

Popular posts from this blog