R.KELLY KUIKANYAGA TANZANIA

Mwimbaji staa wa dunia Robert Kelly au R. Kelly amethibitisha kuja Tanzania uwanja wa taifa Dar es salaam kufanya show kwenye pambano ambapo Evander amethibitisha kulicheza.

Promota Jay Msangi kutoka Hall of Fame boxing amesema baada ya R. Kelly kuthibitisha kuwa atakuja, wako kwenye hatua za mwisho kumalizia mpango wote.

Msangi amesema tarehe ya pambano la Evander na Francois Botha wa Afrika kusini lilikua lichezwe April 2014 lakini wameifuta hiyo tarehe na sasa linaweza kufanyika mapema kabisa.

Hata hivyo Francois Botha atakuepo Tanzania August 2013 kwa ajili ya kupromote pambano hilo, lakini pia kuhudhuria pambano la Francis Cheka na Mmarekani Derrick ambapo litakua la kihistoria kwa mara ya kwanza kwa mtanzania kuzichapa na Mmarekani hapa Tanzania.

Hall of Fame boxing ni kampuni yenye mkono wa Watanzania na Wamarekani, ambapo inao uzoefu wa kuandaa mapambano nchini Marekani lakini sasa watakua wanafanya na Tanzania pia.


Popular posts from this blog