MUGABE KUAPISHWA LEO

Rais wa Zimbabwe, Robert Gabriel Mugabe, anaapishwa rasmi leo kwa awamu ya saba kama kiongozi wa taifa hilo, ikiwa ni siku chache baada ya mahakama nchini humo kuthibitisha matokeo ya uchaguzi uliofanyika tarehe 31 mwezi uliopita, ambao matokeo yake yalipingwa na mpinzani wake, Morgan Tsvangirai. Chama cha Tsvangirai, cha Movement for Democratic Change, MDC, kitasusia sherehe ya kuapishwa kwa Mugabe katika uwanja wa mpira mjini Harare.


Share: