Malalamiko hayo ya wakulima yamekuja kufuatia tukio la ngombe
za wafugaji kuuawa ambapo wakulima hao wametupia lawama jeshi la polisi
kushindwa kuondoa mifugo katika maeneo ya wakulima kama ilivyoagizwa na serikali
ya wilaya na kuwatuhumu askari kutumia nguvu kutawanya maandamano na baadhi ya
wakulima kushikiliwa na jeshi la polisi.
Akizungumzia tuhuma hizo mkuu wa kituo cha polisi Turia Rajab
Shemndolwa amesema wamelazimika kutumia nguvu kutokana na wananchi kutofuata
taratibu za kufanya maandano na kukaidi amri ya jeshi na kwa kufunga barabara
kwa mawe kwa zaidi ya masaa manne na kuzuia shughuli za usafiri.
Nae mkuu wa wilaya ya Mvomero Antony Mtaka akizungumzia tuki
hilo amekiri uharibifu mkubwa uliofanywa baada ya mahindi kuliwa na mifugo hali
inayosababisha njaa kwa wakulima waliolima lakini kuwa mkakati wa serikali sasa
ni kusikiliza malamiko ya pande zote mbili katika kutatua mgogoro huo.